Wakazi wa Kata ya Nyasaka iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wamehimizwa kulinda miundombinuu ya jengo jipya la ofisi ya kata hiyo ili liweze kuwahudumia na kuwasaidia katika utatuzi wa kero pamoja na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika jamii.
Rai hiyo imetolewa na Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 Ndg. Ismail Ali Ussi wakati akizindua mradi huo wa jengo la ofisi ya Kata pamoja na kukabidhi kompyuta na printa vyenye thamani ya shilingi Mil. 3.3 siku ya tarehe 26.08.2025 huku akiwasisitiza watumishi wa kata hiyo kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi
Pia amewakumbusha wakazi wa kata hiyo na jamii kwa ujumla kuwasilisha changamoto zao katika ngazi ya awali ambayo ni ofisi ya serikali ya mtaa kabla ya kuzipeleka katika ngazi za juu kwani utatuzi wa changamoto na masuala mbalimbali katika jamii kuanzia ngazi za chini.
Akisoma taarifa ya Mradi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Ilemela, Bi. Rosemary kasanga mtendaji wa kata ya Nyasaka alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia wananchi wa Kata hiyo kupata huduma katika mazingira bora na salama pamoja na watumishi kupata mazingira bora ya kutolea huduma.
Mradi wa Ujenzi huo umegharimu jumla ya shilingi Mil. 119.7 iliyotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.