Wahudumu wa afya ngazi ya jamii kutoka katika vituo 24 vya kutolewa huduma ndani ya manispaa ya Ilemela wamejengewa uwezo ili kuboresha huduma za lishe wilayani humo
Akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wahudumu hao katika ukumbi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mratibu wa Lishe manispaa hiyo Bi Pili Kasimu amefafanua kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuboresha huduma za lishe katika vituo vya kutolea huduma pamoja na kutambua kwa urahisi watoto wenye changamoto ikiwemo udumavu, ukondefu na uzito uliokithiri
'.. Wahudumu wa afya ngazi ya jamii wakijengewa uwezo inakuwa ni rahisi kufanya vizuri katika maeneo yao wanayotolea huduma, Na hili litaboresha huduma zetu tunazozitoa kwa wananchi ..' Alisema
Aidha Bi Pili amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanajitokeza katika vituo vya kutoa huduma za afya pindi wanapoona hali tofauti za watoto pamoja na kushiriki mara kwa mara katika kujua na kufuatilia hali za kiafya za watoto wao
Kwa upande wake muhudumu wa afya kutoka katika kata ya Sangabuye Bwana Makoye Butikila amesema kuwa mafunzo waliyoyapata yamewaongezea ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ya Kila siku huku akiwataka wadau mbalimbali kuona umuhimu wa kuwa na mafunzo ya mara kwa mara badala ya kusubiria mipango ya serikali peke yake
Bi Grace Aloyce Masare kutoka kata ya Buswelu ameishukuru Serikali kwa kuendesha mafunzo hayo kwani alikuwa akitamani Kila siku kupata mbinu mpya zitakazomsaidia katika kutekeleza wajibu wa Kila siku huku akiwaasa wenzake kwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo
Manispaa ya Ilemela imeendesha mafunzo ya siku moja kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili kufanya kwa urahisi wajibu mbalimbali ikiwemo utoaji wa matone ya vitamin 'A', Dawa za minyoo na upimaji wa hali za Lishe katika vituo vya kutolea huduma za afya na lishe
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.