"Manispaa ya Ilemela itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wenye nia njema kwa lengo la kuleta maendeleo ndani ya Wilaya nzima ya Ilemela hii inaenda sambamba na vipaumbele vya serikali ya awamu ya sita kwa kuhakikisha changamoto mbalimbali za wananchi zinapata ufumbuzi kwa wakati."
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mhe. Renatus Mulunga wakati akipokea jumla ya mashuka 50 yenye thamani ya takribani shilingi laki nane katika zahanati ya Nyakato kutoka SACCOS YA NBE ya wafanyakazi wa kiwanda cha soda za cocacola
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo diwani wa kata hiyo Mhe.Jonathan Mkumba ametoa shukrani kwa wafanyakazi hao kwa kuona na kutambua umuhimu wa sekta ya afya ndani ya kata ya Nyakato.
"Huduma za kituo hiki ni nzuri ndo maana tunaendelea kupata wagonjwa wengi hadi kutoka kata za Wilaya jirani ya Nyamagana hivyo nasi hatuna budi kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa hapa zahanati." Mhe.Mkumba
Kwa upande wake Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Bwana David Otieno amefafanua kuwa vifaa walivyotoa ni utekelezaji wa agizo namba Saba la Sheria na taratibu za vyama ushirika nchini la kutaka kutengwa fedha kwaajili ya shughuli za kijamii na kwamba zoezi hilo litakuwa endelevu hivyo kuviomba vyama vyengine vya ushirika kuiga mfano huo
Nae Afisa ushirika wa Manispaa Bi. Teddy Chrisant ametoa rai kwa SACCOS zingine kuendana na kanuni za ushirika kwa kuhudumia jamii pindi vyama vinapotengeneza faida.
Grace Ngongo ni muuguzi katika zahanati ya Nyakato yeye anatoa shukrani kwa uongozi wa NBE SACCOS kwa msaada huo wa mashuka kwa ajili ya wateja wao.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.