Wadau mbalimbali ndani ya Wilaya ya Ilemela wanaendelea kuhamasika katika shughuli za maboresho ya miundo mbinu inayohusu sekta ya elimu.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi 1 na matundu 7 ya vyoo unaotekelezwa na mdau Auric air services wanaojishughulisha na usafiri wa anga Mhandisi Vita Masonga kutoka kampuni hiyo amesema lengo kuu la mradi ni kupunguza uhaba wa miundo mbinu ya madarasa na vyoo uliopo shule ya msingi Mwambani inayopatika ndani ya kata ya Ilemela.
"..tumemsikia mara kadhaa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela akihamasisha maendeleo, nasi tukaona tunayonafasi ya kufanya kitu hapa shuleni katika kipengele chetu cha kutoa kwa jamii.." Mwalimu Remmy Sagawala ni Mkuu msaidizi katika shule ya msingi Mwambani ameainiasha manufaa punde mradi huo utakapo kamilika ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa wanafunzi katika vyumba vya madarasa, mazingira yatakuwa wezeshi kwa walimu na wanafunzi hali itakayopelekea kuwepo kwa ufaulu mzuri.
Nae mhandisi Juma Matanga kutoka Manispaa hiyo amesema watashirikiana na mdau huyo kuanzia mwanzo wa ujenzi mpaka mwisho katika kuhakikisha kinapatikana kitu kizuri kwa viwango vinavyokubalika .
Akimwakilisha Afisa elimu msingi Mwl.John Johaness amepongeza juhudi za ujenzi huo unaoendelea huku akizidi kualika wadau zaidi kuona mahali watakapoweza kuongeza nguvu ili kuongeza kasi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Ilemela huku akisadifu kauli mbiu ya Wilaya hiyo isemayo 'Ilemela ni yetu tushirikiane kuijenga '
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.