Jumla ya vyama 15 vya siasa vilivyosajiliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini vinatarajiwa kushindana katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024 ndani ya wilaya ya Ilemela siku ya tarehe 27 novemba 2024.
Taarifa hiyo imetolewa na msimamizi wa uchaguzi wa serikali za Mitaa Bi Ummy Wayayu alipozungumza na vyombo vya habari siku ya jumapili tarehe 17 Novemba 2024 kwa ajili ya kutoa muelekeo wa hali ya uchaguzi katika manispaa ya Ilemela.
Bi Ummy alifafanua zaidi kwa kuvitaja vyama hivyo 15 ambavyo vimekidhi vigezo na kusimamisha wagombea katika uchaguzi kuwa ni CCM, CHADEMA, ACT-WAZALENDO, SAU, UMD, CUF, UPDP, NCCR, CCK, DP, UDP, AAFP, DEMOKRASIA MAKINI, ADC na NLD
Aidha baada ya rufaa zote zilizowasilishwa na kutolewa uamuzi manispaa ya Ilemela itakuwa na jumla ya wagombea 1798 ambapo kati yao wagombea 373 ni wa nafasi ya uenyekiti na wagombea 1425 ni kwa nafasi ya ujumbe wa kamati ya mtaa kundi mchanganyiko na kundi la wanawake ambao wameteuliwa kushiriki uchaguzi huo alisema Bi Ummy.
Viongozi wa vyama vya siasa wilaya ya Ilemela wamepongeza kwa namna ambavyo msimamizi wa uchaguzi manispaa ya Ilemela amekuwa akiwashirikisha kuanzia hatua za awali za uchaguzi huku wakishukuru kwa namna mchakato wa uchaguzi ulivyoendeshwa kwa uwazi.
Bi Rebecca Samson Mwita ambae ni Katibu wa wilaya kutoka chama cha Democratic Party akiwapongeza wanawake kwa kujitokeza kugombea na kwamba chama chake kimetoa nafasi sawa kwa jinsia zote ikiwa ni pamoja na kuzuia rushwa za ngono kwa jinsia ya kike
Nae Bwana Holela Mabula ambae ni katibu wa chama cha kijamii CCK wilaya ya Ilemela amempongeza manispaa ya Ilemela kwa maandalizi mazuri ya uchaguzi na ushirikishwaji kwa vyama vya siasa
Bi Ummy Wayayu alihitimisha kwa kuwasisitiza wananchi kujitokeza katika mikutano ya kampeni kwa ajili ya kusikiliza sera za vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo ili kufanya maamuzi sahihi siku ya kupiga kura na kuwachagua viongozi watakaoweza kuwatumikia kwa uadilifu na kuwaletea maendeleo katika mitaa yao, huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarab ili kudumisha amani iliyopo
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.