Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2025 Ndg. Ismail Ali Ussi kwa Vijana wa Bodaboda na bajaji kupitia Klabu ya wapinga rushwa kikundi cha G - 4 Ant Corruption Ambassadors kilichopo Kata ya Buswelu, Halmashauri ya manispaa ya Ilemela.
Vijana hao walipatiwa mafunzo maalum ya kupambana na kudhibiti rushwa kupitia Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU).
“Ombi langu kwenu, nendeni mkafanye uadilifu kupitia mafunzo mliyopatiwa, maafsa hawa ambao mnawaona leo hii wa TAKUKURU wanaendelea kutimiza wajibu wao kwa uadilifu hivyo igeni mfano kwao, msiende kumbamkia mtu kesi ambayo hamna uhakika nayo.
Klabu hiyo ya wapinga rushwa ilianzishwa mnamo Julai 2025 ikiwa na idadi ya wanachama (wanaume) 15 na hadi Agosti 2025 wanachama wameongezeka kutoka 15 hadi wanachama 20, kwa lengo la kusaidia maafisa usafirishaji wa bajaji na bodaboda waweze kufahamu madhara ya rushwa na kupambana nayo.
Wilaya ya Ilemela imeendelea kuzuia na kupambana na rushwa kwa kuelimisha wananchi juu ya athari za kuomba na kupokea rushwa, mathalani kwa kufungua na kuimarisha vilabu vya wapinga rushwa katika shule za Msingi, Sekondari, Vyuo na makundi rika ndani ya Wilaya.
“KUZUIA RUSHWA NI JUKUMU LAKO NA LANGU TUTIMIZE WAJIBU WETU”
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.