“Ombi langu kwenu, endeleeni kuunga mkono na kuthamini jitihada za serikali, kwa bidii hii mliyoionyesha sisi kama serikali tupo tayari kuendelea kuwashika mkono zaidi na zaidi katika kuhakikisha mradi huu unasonga mbele ikiwemo kuwapatia tenda mbalimbali”
Ni kauli ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2025 Ndg Ismail Ali Ussi alipotembelea kikundi cha vijana cha CROSSOVER siku ya tarehe 26/08/2025 kwa lengo la kukagua maendeleo ya kikundi hicho ambacho ni moja ya wanufaika wa mkopo wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya manispaa ya Ilemela ambapo amewapongeza kwa kuweza kuutumia mkopo huo kwa malengo yaliyokusudiwa na hatimaye kuwaletea manufaa.
Aidha Ndg. Ussi, amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza azma yake ya kuwainua wananchi kiuchumi kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwenda kwenye makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Naye mwenyekiti wa kikundi cha CROSSOVER FOUNDATION Ndg. Gerald James Masso akisoma taarifa ya mradi wa kikundi chao amesema kuwa kupitia mkopo huo wamefanikiwa Kutoa ajira kwa vijana wanne (4) pamoja na wanakikundi 05 na pia mradi unachangia mapato ya Serikali kwa kulipa kodi za moja na kwa kupitia bidhaa zinazonunuliwa madukani.
“Tunamshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassankwa kuendelea kuwawezesha kiuchumi makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.” Alimalizia Mwenyekiti huyo.
CROSS OVER FOUNDATION ni kikundi kilichopata shilingi milioni 50 kutoka manispaa ya Ilemela ambacho kinajishughulisha na uchapishaji wa mabango, vifungashio, note book, uchapaji wa stika, nembo na chapa katika vifaa mbalimbali kama magari, vigae, vikombe, nguo na picha kwa teknologia ya kidigitali.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.