Rai imetolewa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 Ndg. Ismail Ali Ussi kwenda kwa vijana kuhakikisha wanazitumia fursa za kiuchumi zinazopatikana ndani ya manispaa ya Ilemela ikiwa ni pamoja na mikopo inayotokana na asilimia 10 ya makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri ili kujikwamua kiuchumi.
Ndg Ussi alitoa rai hiyo siku ya tarehe 26 Agosti alipokuwa akifunga kongamano la vijana lililofanyika viwanja vya Nyamhongolo likilenga kujadili fursa za kiuchumi, uadilifu, uongozi, malezi na makuzi, afya ya uzazi na jamii, stadi za maisha, kushiriki uchaguzi mkuu na uzalendo kwa Taifa.
“Dhamira ya kuanzisha makongamano haya kwenye mbio za mwenge wa uhuru ni kuyaenzi maono ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa ni kiongozi aliyeweka heshima kubwa kwa wananchi anaowatumikia kwa kuongeza fursa za kujiinua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuzielekeza Halmashauri kutumia asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa vikundi vya Wanawake, Vinaja na watu wenye ulemavu.” Alisema mkimbiza mwenge huyo.
Vile vile Ndg. Ussi alihamiza vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu kwa amani na utulivu kama ambayo kauli mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu inavyosema “JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU”
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.