Vijana wa kitanzania wamehamasishwa kujiajiri katika sekta ya kilimo kwani sekta yenye fursa nyingi za kujikwamua kiuchumi na yenye masharti nafuu katika uendeshaji wake badala ya kutegemea kuajiriwa pekee
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa divisheni ya kilimo, mifugo na uvuvi wa manispaa ya Ilemela Bi Neema Semwaiko wakati wa ziara ya mafunzo ya wanafunzi wa mwaka wa pili idara ya jiografia na mazingira kutoka chuo kikuu cha Dodoma ambapo amewataka vijana kuziona fursa zilizopo katika kilimo na kuitumia sekta hiyo kama mbadala wa ajira na kujiingizia kipato
‘.. Tumewapitisha vijana kwenye maeneo mbalimbali ya mijini ambapo wamejionea namna kilimo kinavyoweza kufanyika mijini na ukapata chakula na fedha, Wamekutana na vijana wenzao ambao wanalima na wanajipatia fedha, Kusoma sio lazima uajiriwe unaweza ukasoma na ukajiajiri kwenye kilimo na ukaendesha maisha yako vizuri ..’ Alisema
Aidha Bi Semwaiko ameongeza kuwa Serikali imekuwa ikiwekeza fedha nyingi katika sekta hiyo ikiwemo mafunzo na uanzishwaji wa benki ya kilimo TADB ambayo kwa kiasi kikubwa inasaidia wakulima hasa katika kujipatia mitaji hivyo kuwaomba vijana kujikita katika sekta hiyo
Daktari Enock Makupa ni mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dodoma ambapo mbali na kuishukuru manispaa ya Ilemela kwa ushirikiano kwa wanafunzi wake katika kufanya utafiti na kujifunza kwa vitendo wakati wa ziara yao ndani ya manispaa hiyo, ameongeza kuwa lengo kuu la ziara yao mbali na kujifunza pia ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuwaanda vijana kuanza kufikiria namna bora ya kuajiri badala ya kufikiria ajira za serikali peke yake huku akiwaasa vijana kubaini fursa zilizopo katika jamii sanjari na kuyatumia matatizo yaliyopo kuwa fursa
Donesphory Sebarua na Prisca Dotio Francis ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma idara ya geografia na mazingira kwa nyakati tofauti wamesifu utaalam wa ulimaji wa kisasa kwa kutumia eneo dogo kwa maeneo ya mjini unaojulikana kama KICHUGUU CHA JIKONI waliokutana nao kutoka kwa moja ya wakulima wa manispaa ya Ilemela ambapo wameongeza kuwa kupitia utaalam huo wameweza kushawishika na kuanza kufikiria kujiajiri na kujiongezea kipato pindi atakapomaliza masomo yao huku wakisisitiza vijana wenzao kufikiria na kuziona fursa zilizopo ndani ya sekta ya kilimo
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.