Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024, viongozi wa dini, wazee maarufu na wazee wa kimila katika halmashauri ya manispaa ya Ilemela wametakiwa kuyafikia na kuhimiza amani kwa makundi mbalimbali katika jamii zao.
Wito huo umetolewa na msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa Ilemela, Bi Ummy Wayayu siku ya tarehe 18 Novemba 2024 alipokutana na kundi hilo kwa lengo la kuwapa muelekeo wa uchaguzi kwa maana tulipotoka, tulipo na tunapoelekea
“Niwaombea mkahimize amani misikitini, makanisani kwenye makundi mbalimbali yanayotuzunguka, tunatamani sana uchaguzi uende kwa amani na utulivu”. Alisema Bi Ummy
Sambamba na kuhimiza amani amewataka kuwahamasisha wananchi wa Ilemela kushiriki kampeni za wagombea zitakazoanza tarehe 20 hadi 26 Novemba 2024 ili wakasikilize sera za wagombea hao ili waweze kuchagua viongozi watakaowafaa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Kundi hilo limeshukuru kwa namna ambavyo wamekuwa wakishirikishwa, ambapo Abdulwarith Abdallah ambae ni Shehe wa Wilaya ya Ilemela na Mwenyekiti mwenza wa kamati ya Amani ya wilaya, kwa niaba yao alisemma kuwa wataendelea kuhimiza amani hususan katika nyumba za ibada, pamoja na jamii inayowazunguka.
“Tutaendelea kuhimiza amani popote tutakapokuwa na kuyafikia makundi mbalimbali katika jamii zetu na kila mmoja anapotoka hapa atoke na sera ya amani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa”. Alisema Shehe Abdulwarith
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.