Ukarabati wa kituo cha afya Buzuruga unatarajiwa kukamilika ifikapo mwisho wa mwezi wa kwanza 2019 hii ni kwa mujibu wa mhandisi wa ujenzi Mhandisi Maloba ambapo amesema kuwa hadi sasa ukarabati umefikia takribani asilimia 95 za ukamilishaji na kuwa wapo hatua za ukamilishaji wa ujenzi wa mfumo wa maji machafu.
Mradi huu wa ukarabati ambao unalenga kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi hasa wakati wa dharura (0bstetric Emergencies) umehusisha ujenzi wa majengo matano ambayo ni jengo la wodi ya wakina mama, jengo la kutunzia maiti(mortuary), nyumba ya mtumishi, jengo la maabara na jengo la kufulia (laundry).
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Manispaa, Daktari Tinuga amesema kuwa wananchi wameshirikishwa katika mradi kwani pamoja na kuwa na kamati mbalimbali kama kamati ya afya ya kituo kamati ya manunuzi , kamati ya mapokezi na kamati ya ujenzi, jumla ya wananchi 97 waliajiriwa kama vibarua katika mradi huu wanawake wakiwa 35 na wanaume 62.
Aliongeza kuwa, wananchi wa kata zinazozunguka kituo hiki pia wamehamasishwa kupitia vikao vyao vya maendeleo za kata ili kuchangia ujenzi wa fensi ya kuzunguka eneo la kituo na uhamasishaji unaendelea.
Mradi huu ni kati ya miradi 97 katika awamu ya nne ya ukarabati na uboreshaji wa vituo vya afya ili viweze kutoa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito ambapo fedha kiasi cha Tshs. 400,000,000.0 ziltolewa na serikali kuu kwa kituo hiki mwishoni mwa mwezi Juni 2018.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.