Timu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI na wadau wa Maendeleo (USAID) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3+) Ikiongozwa na Dkt. Enoch Nyanda Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Uchumi na Uzalishaji OR- TAMISEMI wamefika Ilemela kwa lengo la kufuatilia namna mifumo ya TEHAMA inavyoboresha utoaji wa huduma kwa jamii toka ianze kutumika
Katika ziara hiyo ya kikazi ambayo itadumu kwa siku 3, timu hiyo imeweza kufanya ufuatiliaji katika Shule ya Sekondari Buswelu na kukagua namna mfumo wa FFARS unatumika pamoja na Kituo cha Afya Buzuruga ambapo wameangalia matumizi ya mfumo wa GoTHOMIS
“Tumefika Ilemela kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ambayo imefadhiliwa na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3+) sambamba na kuangalia namna ya kuboresha changamoto zote zitakazojitokeza Pamoja na hilo tutakagua baadhi ya vituo vya afya, shule, ili kuona namna halmashauri inatekeleza shughuli mbalimbali kupitia mifumo mbalimbali ya TEHAMA kama vile GoTHOMIS, PLANREP, FFARS n.k Lengo ikiwa ni kuona namna gani mifumo ya TEHAMA inavyoboresha utoaji wa huduma kwa jamii toka ianze kutumika” Amesema Dkt. Enock Nyanda Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Uchumi na Uzalishaji OR- TAMISEMI
Ameongeza kusema kuwa pamoja na kukagua matumizi ya mifumo hiyo pia wataweza kusikiliza changamoto zinazowapata wanaotumia mfumo huo kwa lengo ya kuzitatua.
Serikali kwa kushirikiana na wadau kama USAID wameendelea kurahisisha utendaji kazi kwenye shughuli za kila siku kwa kuleta mifumo rahisi kwenye usimamizi ambayo imekua ikirahisisha kuchakata na kuunganisha taarifa katika ngazi zote za utendaji kuanzia Vijijini hadi Taifa.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.