Ujenzi wa vyumba 110 vya madarasa katika shule za Sekondari za Manispaa ya Ilemela umefikia takriban asilimia 80 ya ukamilishaji, ambapo kukamilika kwa ujenzi huu kunaenda kuondoa changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa kwa shule za sekindari
Hilo limebainishwa katika ziara ambayo imeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela ambayo ameifanywa kwa takriban siku tatu ikiwa na lengo la kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa madarasa hayo ikiwa ni pamoja na kukagua ubora wa ujenzi kwa kulinganisha na thamani ya fedha.
Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masala ameendelea kumshukuru Mhe Rais kwa kutoa kipaumbele katika sekta ya Elimu huku akiwapongeza wasimamizi wote kwa usimamizi mzuri na kusema kuwa anatarajia kuwa ujenzi utakamilika kwa wakati.
",Matarajio ni kuwa tumekamilisha ujenzi wa madarasa haya 110 kufikia tarehe 15 Disemba 2022 na kuyakabidhi madarasa haya kwa Mkuu wa Mkoa ili aweze kumkabidhi Mhe. Rais", Amesema Mhe Masala
Aidha ametoa wito wa kuanza kufikiria ujenzi wa maghorofa kwani maeneo yameanza kuwa finyu hali itakayopelekea kwa siku za mbeleni kuwakosesha wanafunzi maeneo ya kucheza.
Nao Waheshimiwa Madiwani kutoka kata ambazo ujenzi wa madarasa unaendelea wameahidi kuendelea kuunga juhudi za Mhe.Rais kwa kusimamia vizuri miradi yote ya maendeleo.
Walimu kutoka shule za Sekondari kwa nyakati tofauti wametoa shukurani kwa serikali ya chini ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu katika sekta mbalimbali hususan elimu kwani inaenda kuboresha Mazingira ya Kujifunza na Kujifunzia
Ikumbukwe mnamo mwezi Septemba Mhe Rais aliipatia Ilemela kiasi cha Shilingi Bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 110 vya madarasa katika shule za sekondari 23 kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023,
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.