Kukamilika kwa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Kahasa iliyopo kata ya Ilemela, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kutasaidia kuondoa changamoto ya utoro wa wanafunzi.
Akielezea manufaa ya kukamilika kwa mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Mwl. Aristides Mutalemwa Francis amesema kuwa licha ya vitendo vya utovu wa nidhamu kwa wanafunzi ikiwemo utoro kupungua lakini pia mradi huo utawawezesha wanafunzi wanaohitimu darasa la saba katika kata ya Ilemela kupata elimu katika mazingira rafiki na pia utapunguza msongamano wa wanafunzi katika shule za jirani.
Ameyasema hayo akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa shule hiyo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ndg. Ismail Ali Ussi wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Naye Ndg. Ismail Ali Ussi, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 ameupongeza uongozi wa Wilaya pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kutoa fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na kukamilisha ujenzi ukiwa katika ubora na viwango vya hali ya juu”
Mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Kahasa kwa awamu ya kwanza umegharimu shilingi Milioni 400 ikijumuisha ujenzi wa vyumba nane (8) vya madarasa, maabara mbili (2) za sayansi, jengo moja (1) la utawala, matundu kumi ya vyoo vya wanafunzi na kichomea taka 1 na hadi kukamilika unatarajia kugharimu kiasi cha shilingi Mil. 584 ukikamilisha maabara 1 ya sayansi, chumba cha TEHAMA, Maktaba, matundu 6 ya vyoo vya walimu na tanki la maji.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.