Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inatarajia kuongeza ukusanyaji wa mapato yake ya ndani mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mzani wa Mwaloni Kirumba.
Pamoja na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani, kukamilika kwa mradi huu kutasaidia kuboresha takwimu ambazo kimsingi husaidia sana katika kufanya maamuzi mbalimbali ya Halmashauri na Taifa kwa ujumla juu ya Sekta yetu ya Uvuvi pia itasaidia kuondoa migogoro na wafanyabiashara, na taasisi nyingine za serikali zinazosimamia tozo na uzani wa mizigo.
Katika bajeti ya mwaka 2017/18, Halmashauri ilitenga jumla ya Tshs. 260,712,819 kutoka katika mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa mzani katika soko la samaki la kirumba.
Utekelezaji wa mradi huu ulianza tarehe 22/11/2017 na ulitarajiwa kukamilika tarehe 22/02/2018. Hata hivyo, mradi huu haukukamilika kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali, ikiwemo kubadili eneo la ujenzi ambako kulisababisha kuongezeka ukubwa wa kazi kutokana na aina ya udogo. Hadi sasa, utekelezaji uko asilimia tisini (90%) na unatarajiwa kukamilika mwezi huu Tano.
Mwalo wa Kirumba una upekee wake kwa kuwa ni tofauti na mialo mingine, kwani eneo hili ni soko mama la kibiashara ambalo hupokea mazao ya samaki na jamii yake ya ziwa Victoria kutoka sehemu mbalimbali, ndani na nje ya Manispaa ya Ilemela na nchi kwa ajili ya kuuzwa.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.