• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

TUMIENI MABARAZA YA WAZEE KUISHAURI SERIKALI- DC ILEMELA

Posted on: November 28th, 2018

Wazee wa Ilemela pamoja na wazee wote nchini, watakiwa kuyatumia mabaraza yao yaliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria  kuishauri Serikali katika kutekeleza mambo ya msingi ya kujiletea maendeleo.


Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Severine Lalika wakati akizindua baraza la wazee la Wilaya ya Ilemela ,ambapo amewataka wazee hao kuwa sehemu ya serikali sanjari na kuwa mwarobaini katika kufichua na kutafuta suluhu ya changamoto zote zinazokwamisha utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo ikiwemo ukusanyaji wa mapato na mmomonyoko wa maadili.

‘…Nyie ni wadau wa maendeleo hivyo mnao wajibu wa kuishauri Serikali katika nyanja mbalimbali, zikiwemo za kisiasa, kijamii na uchumi..’ Alisisitiza


Aidha amewapongeza viongozi wote waliochaguliwa kuongoza baraza hilo sambamba na kuwahakikishia ushirikiano huku akiahidi kukutana nao tena haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kujadiliana kwa pamoja juu ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo.


Akimkaribisha Mkuu wa Wilaya,  Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Ndugu Said Kitinga alisema kuwa,  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa na desturi ya kukutana na wazee na kubadilisha nao mawazo juu ya mambo mbalimbali ya kijamii katika awamu zote za uongozi  tangu kupata uhuru mpaka awamu ya sasa hatua inayodhihiridha juu ya umuhimu wa kundi hilo katika jamii.


Kwa upande wake mratibu wa baraza la wazee wilaya ya Ilemela Bi Neema Kavishe ametaja umuhimu wa kuanzishwa kwa baraza hilo ikiwemo kutumika na Serikali, wasiasa, watendaji na taasisi kama chanzo cha habari na sehemu sahihi  ya kupata takwimu za wazee kabla ya kupanga mipango ya kimaendeleo inayohusu wazee.


Nae Mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya ya Ilemela Shehe Mohamed Yusuph,  mbali na kuupongeza uongozi wa wilaya ya Ilemela kwa ushirikiano wanaoutoa kwa wazee hao, ameishukuru Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais Daktari John Pombe  Magufuli kwa kulithamini kundi hilo katika jamii na kuamua kuanzisha utaratibu wa kupata matibabu ya huduma za afya bila malipo kwa kutumia kadi maalumu huku akiahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza shughuli za kimaendeleo.

Baraza la wazee la Wilaya ya Ilemela liliundwa mnamo tarehe 22/09/2018 ambapo Shehe Mohamed Yusuph Hasan alichaguliwa kuwa Mwenyekiti huku , Makamu Mwenyekiti akiwa Bibi. Prisca Mwisijo, Katibu Ndibai Yukao, Katibu Msaidizi Jackson Kabote, Mweka Hazina Ndugu Daniel Makorere pamoja na wajumbe wawili wakiwakilisha upande wa wanaume na wanawake ambao ni Bwana Saulo Mihigo na Bibi Mary Masalu


Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • WALENGWA TASAF WAASWA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA VIKUNDI

    April 28, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.