Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Adv Kibamba Kiomoni amewataka watendaji wa kata na mitaa kuhakikisha wanasimamia vyema ukusanyaji wa Mapato.
" Nimewaita kuwakumbusha wajibu wangu na wa kwenu wa kuhakikisha tunasimamia vyema ukusanyaji wa mapato", Adv Kibamba
Ameongeza kusema kuwa anaamini wakishirikiana na wenyeviti kazi ya kukusanya mapato itakuwa nyepesi.
Sambamba na hilo amewaelekeza watendaji kuhakikisha wanaweka orodha ya biashara zilizopo kwenye kata pamoja na mawasiliano ya wafanyabiashara, huku akiwataka kuwasilisha taarifa ya makusanyo kutoka kila ijumaa.
Nao Watendaji wa kata na mitaa wameahidi kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na kuhakikisha kuwa watasimamia ukusanyaji wa mapato
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.