Katika kuhakikisha kuwa jamii ya Ilemela inakuwa salama kiafya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kupitia idara ya afya imeanza mikakati ya kuchukua tahadhari ya ugonjwa hatari wa kipindupindu kwa kujadili na kutoa mapendekezo yatakayoleta matokeo chanya na kuiepusha Ilemela katika janga hilo .
Akizungumza wakati wa kikao cha dharura kilichojumuisha maafisa afya wa kata zote za Manispaa hiyo Mganga Mkuu wa Manispaa Dkt.Samson Marwa amesema ni muhimu wataalam wa afya kuendelea kuelimisha jamii juu ya masuala ya usafi hasa hasa wakati wa maandalizi ya vyakula.
"Huu ugonjwa unasababishwa na watu kula kinyesi kupitia vyakula,tuwaambie watu wetu waboreshe usafi wa mazingira yote hasa kipindi hiki cha mvua ili wale chakula kisichokuwa na vimelea wa aina yoyote." Dkt. Marwa
Maeneo yaliyotajwa kuchukua tahadhari zaidi ni maeneo ya masoko,stendi, majumbani sehemu ambako vyakula vinaandaliwa sambamba na kuzingitia usafi wa vyoo hasa maeneo ya mikusanyiko kama mashuleni.
Akiwasilisha mada juu ya tahadhari hiyo mganga mfawidhi wa hospitali ya Wilaya Dtk.Mayunga Mateso ameainisha njia za kuzuia kipindupindu ambazo ni Upatikanaji wa maji safi na salama,kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula na kufunika chakula ili inzi wasitue juu yake.
"Mpaka sasa bado hatuna kesi yoyote ya mgonjwa wa kipindupindu ndani ya Manispaa yetu japo tunafahamu yapo maeneo ya jirani ambako tayari ugonjwa upo ndo maana halisi ya tahadhari hii.Tuchukue tahadhari kipindupindu kinaua." Dkt.Marwa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.