Timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imefanya ziara kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha robo ya pili ( Octoba-Desemba) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Ziara hiyo imeongozwa na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi.Neema Semwaiko,wakiwa shule ya sekondari Lumala iliyopo kata ya Ilemela kukagua ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa yaliyotengewa jumla ya shilingi milioni 24 ya mapato ya ndani ya Manispaa hiyo amesema ni wajibu wa wataalam kila mmoja kutimiza wajibu wake ili miradi yote ikamilike kwa wakati.
"..tunatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani hatuna sababu za kuchelewa tena pesa ipo ni utekelezaji tu.."
Aidha timu hiyo ilipata nafasi ya kutembelea shule ya msingi Kitangiri iliyopatwa na madhara ya kuuezuliwa paa na nyufa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mnamo Desemba 12 mwaka huu 2024 na kutoa dira ya namna ya kurejesha hali nzuri ya miundo mbinu iliyoharibiwa .
Miradi 11 iliyopewa fedha kiasi cha shilingi milioni 240 imetembelewa ikiwemo ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya sekondari Angeline Mabula katika kata ya Kiseke na ujenzi wa barabara ya Mawe Kigoto iliyopo kata ya Kirumba.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.