Kaya 5848 za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela zimeendelea kunufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiwa na TASAF awamu ya tatu kipindi cha pili ambapo zaidi ya Tsh. Milioni 290 zimetolewa kwa kaya hizo.
Mratibu wa TASAF Manispaa ya Ilemela ndugu Frank Ngitaoh amewataka wanufaika wa mpango huu kutumia pesa zao kwa utaratibu mzuri ili ziweze kuwaletea manufaa kwa kuinua uchumi wao huku akiwakumbusha kuwa lengo la mradi huu ni kunusuru kaya maskini na kuwawezesha kukuza kipato cha kaya pamoja na kuendeleza rasilimali watu ameyasema hayo alipozitembelea kaya hizo
“Huu ni mradi wa kunusuru kaya maskini ambao huwa tunafanya kwa kipindi cha miaka mitatu mitatu,wahitaji ni wengi mno ndani ya jamii yetu,nyinyi ambao tayari ni walengwa wa mradi mnapaswa kutumia kipindi chenu vizuri kwa kujiwekeza kidogokidogo kwa kadri mnavyopata angalau kuhakikisha una kitu cha kukusogeza kimaisha.” Amesema Ngitaoh
Pamoja na hayo amewataka walengwa wa mradi huu kuunda na kuboresha vikundi vyao kwa kubuni shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazoweza kuwaletea nafuu ya maisha.
Salome Yuve Yohana ni mmoja wa wanufaika wa mpango wa kunuru kaya maskini Ilemela katika mtaa wa Nyamiswi ndani ya kata ya Sangabuye amesema kuwa toka aingie kwenye mpango anaona utofauti wa maisha aliyokuwa nayo awali na sasa.
“Kipindi cha nyuma hata kupata chakula mara tatu mimi na wajukuu zangu ilikuwa taabu,nashukuru serikali kwa kutuo na na kutuwezesha angalau kujimudu wenyewe kwa kiasi” amesema
Ameongeza kusema kuwa alijiunga, kwenye kikundi na walengwa wenzake mtaani kwao ambapo wamekuwa wakijishughulisha na ufugaji na kukopeshana pesa ndogondogo pale mwanakikundi anapokuwa katika uhitaji naamini hadi kufikia mwisho wa mwaka nitakuwa na nafuu ya maisha zaidi ya nilivyo sasa.Mungu awazidishie.” Amesema
Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Tshs. Bilioni 1.5 zimepokelewa kutoka TASAF kwa ajili ya kunusuru kaya maskini Ilemela
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.