Mpango wa maendeleo ya jamii (TASAF) imeridhishwa na utekelezaji wa miradi na kuipongeza Halmashauri ya manispaa ya ilemela kwa usimamizi mzuri na utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na mpango wa kunusuru kaya masikini tasaf sanjari na matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika uhawilishaji wa fedha kwa walengwa wa mpango huo
Akizungumza mara baada ya ziara ya kutembelea na kuikagua miradi inayotekelezwa na mfuko wa maendeleo (TASAF), mkurugenzi wa mifumo, tathimini na mawasiliano ambae pia ni mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa TASAF makao makuu ndugu Japhet Boaz amesema kuwa katika mkoa wa mwanza manispaa ya ilemela imekuwa kinara katika utekelezaji mzuri wa miradi pamoja na kuwa na idadi ndogo ya walengwa wanaolipwa fedha taslimu mkononi tofauti na maeneo mengine
'.. Serikali imeweka msukumo zaidi katika matumizi ya mifumo ya kielektroniki, ilemela imechukua hili kwa uzito na msukumo mkubwa sana, zaidi ya asilimia 99 ya walengwa wanahudumiwa kielekteoniki, tunatamani halmashauri nyingine zijifunze katika hili ..' alisema
Aidha ndugu Boaz ameridhishwa na utekelezaji mzuri wa mradi wa zahanati ya mihama uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 221.1 na shule ya sekondari igogwe iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 891.46 na kuongeza kuwa miradi hiyo imezingatia thamani ya fedha iliyotolewa huku akiwataka wananchi wa maeneo hayo kuitumia miradi hiyo ili iwe na tija
Leonard Robert ni mratibu wa TASAF manispaa ya ilemela akitoa taarifa ya utekelezaji amesema kuwa manispaa yake ina walengwa 3450 kati yao walengwa 15 tu ndio wanaolipwa fedha mkono nje ya mifumo ya kielektroniki sawa na asilimia 99.7 na kwamba jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa ili walengwa wote walipwe kielektroniki
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kitangiri Mhe Donald Ndaro Na Mhe William Mashamba diwani wa kata ya Bugogwa mbali na kushukuru kwa fedha za utekelezaji wa miradi katika maeneo yao, wameomba serikali kuendelea kutekeleza miradi inayonufaisha wananchi wa maeneo yao na kutatua kero zinazowakabili ikiwemo miundombinu ya barabara, uzio wa shule na vituo vya afya
Nae bi Sikujua Malumba kutoka kikundi cha upendo kata ya Ilemela na Laurencia Lubigisa kutoka kikundi cha wasikivu kata ya bugogwa wameshukuru kwa miradi iliyotekelezwa kwani imewasaidia kupunguza umasikini kwa ngazi ya familia na kuinua uchumi wao na taifa kiujumla
Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2020 hadi 2024 halmashauri ya manispaa ya Ilemela imepokea kiasi cha shilingi bilioni 2.21 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya afya, elimu,barabara pamoja na kukuza kipato cha kaya, huku shilingi bilioni sita zimepokelewa kuanzia mwaka 2021 hadi 2024 kwa ajili ya malipo ya walengwa wa kaya maskini fedha hizi zimepokelewa kutoka mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF)
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.