SHULE YA SEKONDARI YA BUGOGWA YANUFAIKA NA MGAO WA KOMPYUTA
Shirika la wamisionari la Christian Life World Mission Frontiers kupitia taasisi ya angeline foundation imeipatia shule ya sekondari Bugogwa jumla ya Kompyuta 20 ikiwa ni jitihada za Mhe Mbunge wa jimbo la Ilemela katika kuhakikisha kuwa kila shule katika Manispaa ya Ilemela inakuwa na kompyuta ili kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa mbalimbali pamoja na kujiandaa na Tanzania ya Viwanda.
Rais wa shirika hilo la wamisionari, Mchungaji Dr Paul Kim kutokea Korea Kusini amemuhakikishia Mbunge wa Ilemela kuwa ataendelea kuziunga mkono jitihada zake katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Ilemela huku akiahidi kuwa ataleta wataalam ili waweze kufundisha somo la kompyuta ili kuweza kuta wataalam zaidi kwani nia yake ni kuiona Afrika na Tanzania iliyo bora.
Aliyekuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo Mbunge wa Ilemela Mheshimiwa Angeline L.Mabula alisema kuwa, lengo kubwa la kuwapatia kompyuta hizo ni kuwaandaa vijana kwenda na wakati pamoja na kujiandaa na kuijenga Tanzania ya viwanda.
Pamoja na hayo alisema kuwa, ni matarajio yake kuwa walimu watazitumia kwa kupata habari za kielimu pamoja na kuwafundisha wanafunzi na si kwa matumizi mengineyo.Aidha aliwasihi kuimarisha ulinzi katika shule hiyyo ili kuhakikisha kuwa kompyuta hizo haziibiwi ili kuweza kuwapa imani wafadhili na pia wajiandae kuwapokea walimu watakaoletwa kwa ajili ya kutoa elimu ya kompyuta kama wafadhili hao walivyoahidi.
“Tunapoelekea ni Tanzania ya viwanda hivyo ni muhimu kuwa na ujuzi wa matumizi ya kompyuta hivyo maandalizi yanatakiwa yaanze mapema.Pia nasisitiza vijana muwe makini na kufuatilia yale yanayoelekezwa na viongozi wao pamoja na kuunga juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”,Alisisitiza
Aidha hakuacha kugusia kuhusu suala la mimba huku akiwaasa wanafunzi wa kike kujitunza na kuzingatia elimu kwani ndio suala lililowapeleka hapo shuleni huku akisisitiza kuiunga kauli ya Mheshimiwa Rais kwa asilimia 100 ya kupiga mimba mashuleni.
“Huwezi kusoma ukiwa katika hali hiyo, nawasihi kuanzisha klabu za wasichana kwa ajili ya kuweza kuelimishana na pia walimu muwaone wanafunzi hao kama watoto wenu wa ”, Alisisitiza.
Nae Mheshimiwa Diwani wa kata ya Buswelu ambae ndie Mwenyekiti wa kamati za Huduma za Uchumi, Elimu na Afya pamoja na kuwashukuru wafadhili hao na Mheshimiwa Mbunge kwa kuwapatia kompyuta hizo amewataka wanafunzi wa shule hiyo kuzitunza kompyuta hizo na kusoma kwa bidii ili ziweze kunufaisha na wanafunzi wengine.
Deus Stephano ambae ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo, alimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa jitihada zake na kwa wafadhili kwa kukubali kuwapatia kompyuta hizo. Alisema kuwa kompyuta hizo zitawasaidia kuendana na kasi ya dunia ya sayansi na teknolojia, huku akiahidi kuwa watazitunza ili na wanafunzi wengine watakaosoma katika shule hiyo waweze kuja kuzitumia.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.