Wamiliki wa shule binafsi wametakiwa kujenga uhusiano na jamii inayowazunguka kwa kuhakikisha inashiriki katika kutatua kero, changamoto na utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika maeneo yanayowazunguka ili jamii iweze kunufaika na uwepo wao na kuona kuwa ni sehem yao jambo litakalosaidia kudumisha ulinzi kwa shule hizo kwani litaondoa chuki na uhasama baina ya jamii na shule hizo.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya huduma za Jamii ambae pia ni diwani wa kata ya Nyamhongolo Mhe Andrea Antony Nginila wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kutembelea shule binafsi zilizopo ndani ya Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya kujiridhisha juu ya ubora wa huduma zinazotolewa, uzingatiaji wa sheria, taratibu na kanuni za utoaji elimu.
‘.. Mtakapo shirikiana na jamii katika mambo tofauti wataona nyinyi ni wenzao hata namna ya kuilinda shule itakuwa ni rahisi jamii itawasaidia, Lakini kama hamshirikiani na viongozi wa maeneo yenu, hamshirikiani na jamii ni ngumu kusonga mbele ..’ Alisema
Kwa upande wake Mhe AbdulRahman Simba Diwani wa kata ya Nyasaka ambae pia ni mjumbe wa kamati hiyo amesema kuwa ziara za kushtukiza katika shule binafsi ziwe endelevu kwani zitasaidia kubaini mapungufu ya shule hizo ikiwa ni pamoja na kuzipatia ufumbuzi jambo ambalo litasaidia kuboresha sekta ya elimu ndani ya wilaya.
Nae Mkuu wa idara ya kilimo Manispaa ya Ilemela Bi Neema Semwaiko aliongeza kwa kusema kuwa ipo haja kwa wadhibiti wa ubora wa elimu na maafisa elimu kata kujenga utamaduni wa kutembelea shule zilizopo katika maeneo yao kuzikagua na kuzisimamia vizuri ili zifuate utaratibu unaotakiwa badala ya kusubiria kamati ya huduma pekee kufanya hivyo.
Kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Afisa Elimu msingi Ndugu Marco Busungu ameahidi kuwa maelekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo yataenda kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kuweka msisitizo zaidi katika kuzisimamia shule binafsi badala ya zile za Serikali pekee.
Shule ya msingi PrinceTom na Rorya sekondari kwa kata ya Buswelu, Yusta sekondari na LowJoma shule ya msingi kwa kata ya Nyasaka zilitembelewa.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.