Wawakilishi wa Shirika la Railway Children Africa wamefika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe Hassan kwa ajili ya kutoa taarifa na mwendelezo wa shughuli wanazofanya katika kukabiliana na ongezeko la watoto wa mitaani.
Bi Irene Wampemba ambae ni Meneja Mradi wa Shirika hilo amesema kuwa lengo la shirika hilo ni kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na wimbi kubwa la watoto wa mitaani sambamba na kuhakikisha wanawaunganisha watoto hao na familia zao.
Aidha Bi Irene ameongeza kusema kuwa wanalenga kuimarisha mifumo ya ustawi wa jamii ambayo itawezesha kuendelea kuwatambua watoto wanaoishi mitaani kwa idadi, ambapo hadi sasa shirika hilo limeendelea kuwawezesha maafisa ustawi wa jamii wa Ilemela kuunganisha watoto na familia zao.
Nae Mhe Hassan Masala amewapongeza kwa kazi hiyo ya kujitokea na kuwahakikishia kuwa ameupokea wito huo huku akiwaahidi ushirikiano wa kutosha na kuwa iwapo zipo changamoto zozote zinazowakabili katika utekelezaji wa malengo yao basi wasisite kumshirikisha ili kuwez kupata ufumbuzi.
Aidha Mhe Masala amemuagiza Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Ilemela kuhakikisha anawasilisha mpango kazi hii ikiwa ni pamoja na kuyaalika mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuweza kukutana na kuzijadili changamoto mbalimbali katika jamii hususan msuala ya ukatili.
Dionis Shimbi ni Afisa Utekelezaji wa Shirika yeye ameshukuru kwa kupokelewa na ameahidi kuendeleza ushirikiano na serikali pamoja na wadau wengine ili kuweza kufanikisha malengo yao.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Ilemela Bi Pamela Kijazi, pamoja na kulishukuru shirika hilo la Railway Children Africa kwa maono yao amewahakikishia kuwa wataendelea kushirikiana kikamilifu katika kuwatambua watoto wanaishi na kufanya kazi mtaani na kuwaunganisha na familia zao.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.