Kamati ya fedha na uongozi katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/2025 imekagua miradi ya shilingi Milioni 672.800 fedha kutoka chanzo cha mapato ya ndani ya halmashauri.
Wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mhe Renatus Mulunga wamempongeza Mkurugenzi Ummy Wayayu na wataalam kwa kuelekeza fedha za mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Pamoja na pongezi hizo wamemtaka mkurugenzi kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo inakamilika ili ianze kutumika na kuleta tija kwa wananchi huku wakitoa rai kwa wataalam kutoa ushauri wa kitaalam katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Aidha wajumbe wa kamati hiyo wamesisitiza juu ya ujenzi wa majengo ya ghorofa ili kubana matumizi ya ardhi , ambapo mkurugenzi Ummy alitoa ufafanuzi kuwa kuanzia bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 ujenzi wa ghorofa utazingatiwa.
Miradi iliyokaguliwa tarehe 22 januari 2025 ni ya sekta za afya,elimu, barabara na biashara kati ya miradi hiyo ni ujenzi wa shule mpya, uendelezaji wa ujenzi zahanati, ukamilishaji wa madarasa katika shule za msingi na sekondari, ujenzi wa barabara ya mawe, ofisi za mtaa na kata pamoja na kituo cha kutolea huduma za biashara (one stop center)
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.