Katika kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Ilemela na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla wanatumia vyakula vilivyoongezewa virutubishi ili kutokomeza changamoto ya lishe duni na udumavu, Kampuni ya Kipipa Millers Ltd imewekeza zaidi ya shilingi Bilioni 1.296 katika shughuli za usindikaji wa vyakula vya nafaka na mhogo.
Mradi huo uliotembelewa Tarehe 26. 08. 2025 na mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, shughuli zake kubwa nikuongeza virutubishi katika nafaka za mtama, mahindi pamojana mihogo. Bidhaa huchakatwa, huongezewa virutubishi aina ya asidi ya foliki, vitamini B 12, madini ya chuma na madini ya zinki.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg. Ismail Ali Ussi ameupongeza uongozi wa Wilaya na Halmashauri kwa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuruhusu wawekezaji wa ndani, pia ameipongeza Kampuni ya Kipipa Millers Ltd kwa kuwekeza katika Lishe na kuhakikisha afya za wana Ilemela naTanzania kwa ujumla zinaimarika.
Naye Ndg. Gabriel Abdon Matemu, Meneja wa uzaishaji wakampuni hiyo ameyaelezea mafanikio ya mradi huo kuwa ni pamoja na kutoa ajira za kudumu kwa watu 14 na ajira za muda(vibarua) 12 kwa siku, Jamii, Taasisi za Umma na za Binafsihutumia bidhaa zilizoongezewa virutubishi ambapo jumla yashule 28 kati ya shule 216 sawa na asilimia 13 hununua unga wenye virutubishi ambapo hupata lishe bora na kuimarisha kinga ya mwili.
Pia amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kulipa kipaumbeleswala la Lishe kutoka ngazi ya Taifa hadi Mtaa chini ya kaulimbiu isemayo “Mtaji ni Afya yako, Zingatia unachokula”.
Kampuni ya Kipipa Millers Ltd inauwezo wa kuchakata tani36.5 za nafaka na tani 5 unga wa muhogo ulioongezwa virutubishi.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.