Serikali imedhamiria kuchukua hatua mbalimbali ili kukomesha vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa watoto
Hayo yamesemwa na Ndugu Joachim Otaru akimwakilisha wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kimkoa yaliyofanyika katika viwanja vya Furahisha wilayani Ilemela ambapo amesema kuwa Serikali imehuisha na kuimarisha mabaraza ya watoto katika ngazi za wilaya, kata, mitaa na vijiji ili kutoa fursa ya kuzungumza na kujadili changamoto zinazokabili watoto jambo litakalisaidia kupunguza vitendo vya ukatili
'.. Jumla ya mabaraza 210 yameanzishwa mkoani Mwanza, 1 Kwa ngazi ya mkoa, 8 kwa ngazi ya halmashauri na 154 kwa ngazi ya kata kati ya kata 191 kwa lengo la kuwaweka pamoja watoto ..' Alisema
Aidha Otaru amefafanua kuwa Serikali chini ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan imeimarisha utekelezaji wa mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kuunda kamati za MTAKUWA katika ngazi za kuanzia mkoa, wilaya, kata hadi vijiji
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Ilemela ambae ni katibu tawala wa wilaya ya Ilemela Bi Mariam Msengi mbali na kushukuru na kupongeza kwa sherehe hizo za maadhimisho kufanyika ndani ya wilaya yake, Amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza miradi inayomlenga moja kwa moja mtoto ikiwemo ile ya sekta za elimu na afya
Baraka Kizuri ni mwanafunzi wa darasa la Saba katika shule ya msingi Isenga amesema kuwa maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika ni ukumbusho wa mauaji ya kinyama dhidi ya watoto yaliyowahi kufanyika nchi ya afrika kusini hivyo kilichofanyika leo ni kuikumbusha jamii juu kutetea haki za watoto na kuzilinda
Siku ya mtoto wa afrika Kwa mwaka wa 2023 imepambwa na kauli mbiu ya 'ZINGATIA USALAMA WA MTOTO KATIKA ULIMWENGU WA KIDIJITALI '
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA YALIYOFANYIKA KIMKOA KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA TAREHE 16 JUNI 2023 KATIKA VIWANJA VYA FURAHISHA
Picha Na. 1: Onyesho la Bunge la watoto
Picha na 2: Watoto wa kituo cha SOS wakionyesha onyesho lao
Picha Na. 3: Watoto wakiwa katika maandamano yaliyoanzia eneo la sheli ya Olympic Ghana kuelekea viwanja vya Furahisha
Picha Na. 4:Watoto wa kituo cha SOS wakionyesha onyesho lao
Picha Na. 5: Mwakilishi wa watoto akimsalimia Katibu tawala wa wilaya ya Ilemela
Picha Na. 6Mgeni rasmi akimkabidhi hati ya shukran Afisa maendeleo wa manispaa ya Ilemela Bi Sara Nthangu Kwa niaba ya aliyekuwa afisa maendeleo wa mkoa wa Mwanza Ndugu Ndasa alistaafu hivi karibuni
Picha Na. 7Mgeni rasmi akimkabidhi cheti cha Shukran mwakilishi wa dawati la jinsia kwa wilaya ya Ilemela
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.