Serikali imeahidi kukamilisha ujenzi wa kituo cha polisi Nyamhongolo ili wananchi waweze kupata huduma ya ulinzi na usalama katika umbali mfupi
Hayo yamebainishwa na naibu waziri wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mhe Daniel Sillo alipotembelea wilaya ya Ilemela kata ya Nyamhongolo kukagua ujenzi wa kituo kipya cha polisi ambapo akasema kuwa Serikali inaompango wa kukamilisha vituo 77 vya polisi vilivyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi katika maeneo mbalimbali nchini '.. Niwahakikishie kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais tunaenda kukamilisha vituo vya polisi vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi na hiki kama hakipo tutaona namna ya kukimalizia Ili tuwashike mkono wananchi waweze kupata huduma ..' Alisema
Aidha Mhe Sirro amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kuchangia ujenzi wa kituo hicho huku akimpongeza Mkuu wa wilaya hiyo na viongozi wenzake kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kumshukuru Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan kwa mradi wa ujenzi wa nyumba za askari katika eneo hilo uliochochea uanzishwaji wa mradi wa kituo cha polisi ameiomba serikali kusaidia jitihada za wananchi katika ujenzi wa kituo hicho kwa kuhakikisha kinamalizika
Mutafungwa W.W ni mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza ambapo amefafanua kuwa ukamilishaji wa kituo hicho ni muhimu kwakuwa utasaidia wananchi kupata huduma katika umbali mfupi pamoja na kupunguza mrundikano katika vituo vingine
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masala akasema kuwa wilaya ya Ilemela iko salama hivyo kulipongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri ya kuimarisha ulinzi na usalama likishirikiana na vyombo vyengine vya ulinzi na usalama sanjari na kuahidi kutatua changamoto ndogo ndogo zilizo ngazi ya wilaya ili kufanikisha ujenzi wa kituo hicho cha polisi
Ujenzi wa kituo cha polisi Nyamhongolo ulianza kutekelezwa Februari 22, 2019 ukiasisiwa na Mbunge wa Jimbo hilo huku changamoto inayoukabili mradi huo ikiwa ni kuongezeka kwa bei ya vifaa vya ujenzi na gharama za ununuzi wa maji .
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.