Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuboresha huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kuimarisha miundo mbinu rafiki kwao.
Hayo yamesemwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ndugu Godfrey Mzanva wakati alipokuwa akizindua bweni kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Buswelu ndani ya Manispaa ya Ilemela.
".. Ulinzi na usalama kwa watoto wenye mahitaji maalum ni jukumu la jamii nzima,serikali tayari imeonyesha njia,pongezi kwa Manispaa ya Ilemela kuendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa kujenga mabweni kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum.."
Akisoma taarifa ya ujenzi wa bweni hilo Mkuu wa shule ya msingi Buswelu Mwl.Wiliherimina Sato amesema mradi huo umegharimu jumla ya shilingi milioni 172,505,000 ambapo shilingi milioni 100 ni pesa kutoka serikali kuu kupitia mradi wa LANES na shilingi milioni 72,505,000 ilitokana na mapato ya ndani ya Manispaa hiyo huku akifafanua kuwa bweni hilo lina uwezo wa kuhudumia watoto 76.
Nae mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe.Dkt.Angeline Mabula amemshukuru Mhe.Rais kwa kutoa fedha nyingi kufanya maendeleo Ilemela huku akiwataka wazazi na walezi kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu ndani.
".. Watoto wetu hapa watakuwa salama na watapata nafasi ya kujifunza vizuri wakiwa shuleni muda wote.."
Swaumu Ally ni mzazi ambae mwanae anasoma shuleni hapo amesema anashukuru serikali kwa kuwakumbuka watoto wao na kuwaboreshea mazingira yao ya kucheza na kujisomea.
Shule ya msingi Buswelu ya watoto wenye mahitaji maalum ina jumla ya wanafunzi 90 ambapo wavulana ni 48 na wasichana ni 42 kati yao wenye usonji ni 9, ulemavu wa akili 43,wasioona 4,viziwi 18 na walemavu wa viungo 16.
|
|
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.