• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Serikali kuendelea kuboresha huduma bora kwa wazee

Posted on: October 2nd, 2021

“Serikali itaendelea kujiimarisha katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wazee kwa kuzingatia umuhimu wa kundi hili katika jamii yetu ya Tanzania”

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Bi.Neema Kipeja katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo huadhimishwa tarehe moja mwezi wa kumi ya kila mwaka.


Aidha alisema kuwa Serikali inatambua kuwa wazee ni hazina katika kuibua na kuchochea shughuli mbalimbali za kimaendeleo kutokana na ushauri mzuri wanaotoa wanaposhirikishwa katika mambo ya kimaendeleo.


Aliendelea kusema kuwa Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuthibitisha kuwajali wazee kwa kuboresha mradi wa kusaidia kaya maskini (TASAF) ambapo wazee wote wenye vigezo wameombwa kujitokeza kwenye ofisi za jirani za serikali ili kutambuliwa na kuingizwa kwenye mpango huo.

Pamoja na hayo, Bi. Neema amewahimiza wazee kuwa na utaratibu wa kwenda kucheki afya zenu mara kwa mara ili kupata huduma stahiki kwa wakati kwani huduma za afya kwa wazee kuanzia miaka 60 ni bure katika vituo vyote vya kutolea huduma.


Kupitia maadhimisho hayo Bi. Neema alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazee hao juu ya UVIKO-19 na kuwataka wazee kuendelea kuchanja, kwani wapo kwenye kundi ambalo ni rahisi kupata maambukizi hayo huku akiwatoa hofu kwamba chanjo hii ni salama kabisa na kuwataka kumuunga mkono Mhe.Rais alieona umuhimu wa kuokoa maisha ya watanzania kwa kupata chanjo hii.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo kiwilaya ndani ya kata ya Bugogwa, Mzee Jackson Kabote ambaye ni  katibu wa baraza la wazee wilaya ya Ilemela amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wazee ikiwa ni pamoja upungufu wa dawa na wa wataalam wa kuhudumia wazee,umaskini uliokithiri kutokana na kipato duni au kutokuwa na kipato kabisa sambamba na wazee kutokupewa kipaumbele kama makundi mengine kama vile wanawake,vijana na walemavu.

Halmashauri ya manispaa ya Ilemela imeungana na Halmashauri nyingine nchini Tanzania kuadhimisha siku ya wazee duniani ikiwa ni kumbukizi ya kila mwaka ya siku ya wazee duniani iliyorasimishwa na shirika la kimataifa (UN)miaka 35 iliyopita,ikiambatana na kauli mbiu ya. “matumizi sahihi ya kidigitali kwa ustawi wa rika zote”.



Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.