Serikali mkoani Mwanza itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale wote wanaojihusisha na mmomonyoko wa maadili .
Hayo yamebainishwa na Ndugu Joachim Otaru kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya familia duniani kwa ngazi ya mkoa katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela ambapo amewataka viongozi wote wa dini na Serikali kukemea wazi wazi mmomonyoko wa maadili pamoja na kusimamia maadili kuanzia ngazi ya familia ili kuwa na jamii na taifa lenye maadili
‘.. Tunapoadhimisha siku ya familia duniani, Tunatakiwa kama familia tukae na kujadili maendeleo yetu pamoja na changamoto tunazokabiliana nazo na pia kutafuta suluhu ya changamoto hizo ..’ Alisema
Aidha wazazi wameaswa kutimiza wajibu wao kwa watoto ikiwemo kuwapatia mahitaji msingi, kumlinda mtoto dhidi ya ukatili, mimba za utotoni, ubakaji na ulawiti, kuzungumza nao mara kwa mara ili kubaini changamoto zinazowakabili ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wakati.
Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Mhandisi Modest Apolinary amesema jamii ina wajibu wa kusimamia maadili yanayokubalika kwa watoto kwa kuhakikisha kuwa wanapata mahitaji yao ya msingi na kufuatiliwa kwa karibu katika makuzi yao ili iwe rahisi kutambua changamoto zozote punde zinapojitokeza.
Kwa upande wake moja ya mchangiaji katika maadhimisho hayo, Bi Jonathan Nyabugumba amewaasa viongozi wa dini kutumia nafasi yao katika kuikemea jamii dhidi ya vitendo vya ushoga na ulawiti huku akiishauri jamii kufichua wanaofanya vitendo hivyo ili visiendelee kujitokeza
Nae mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Kivulini Ndugu Yasin Ally ameishauri Serikali kuchukua hatua katika kudhibiti maeneo yanayochochea vitendo vya mmomonyoko wa maadili katika wilaya ya Ilemela ikiwemo kumbi za usiku za starehe
Maadhimisho ya siku ya familia duniani yamefanyika katika wilaya ya Ilemela kwa ngazi ya mkoa wa Mwanza huku kauli mbiu ikiwa ni “ Imarisha maadili na upendo kwa familia imara.”
MATUKIO KATIKA PICHA MAADHIMISHO YA SIKU YA FAMILIA DUNIANI
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.