Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amemuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela kwa kushirikiana na timu yake ya watalaam kuhakikisha kuwa hoja zilizotolewa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) zinafutwa kabla ya kuelekea katika vikao vya LAAC.
Mhe Mkuu wa Mkoa ametoa maelekezo hayo wakati akiendesha kikao maalum cha baraza la madiwani lililoketi kwa ajili ya kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za seikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na utekelezaji wake ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imepata hati safi.
“Mkurugenzi shirikiana na timu yako kuhakikisha kuwa hoja hizi zilizobaki zinamalizika kabla ya kuelekea katika vikao vya LAAC kwani hizi ni hoja dhaifu ambazo zinaweza kumalizika”. Amesema Mkuu wa Mkoa.
Pamoja na hayo amewataka viongozi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa wanaangalia viashiria vyote hatarishi katika matumizi ya fedha, fedha mbichi isiliwe, miradi yote isimamiwe na kamati za ujenzi huku akiwataka kuhakikisha kuwa mapungufu yaliyojitokeza hayajirudii kwani nia na ndoto ya Mhe Rais Samia Suluhu, ni fedha zitumike na kuleta matokeo chanya katika jamii tunayoisimamia.
“Mafanikio hayaji hivihivi, ni kujituma kwa viongozi niwapongeze wote, Mbunge wa Jimbo, Mstahiki Meya na Baraza lako, timu ya wataalaam kwa kufanikisha haya kutembea pamoja, kutambua changamoto na kuweza kuzitatua na pale inapobidi kujisahihisha, aidha nikupongeze pia Mkurugenzi ambae ni kiongozi wa watumishi kwa kuwa msikivu na kuona kuwa maendeleo yanapatikana Ilemela, Alisisitiza Mhandisi Gabriel
Nae Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Salum Kali amesema kuwa anayo imani kuwa maelekezo yaliyotolewa yatafanyiwa kazi na kuwa mwaka wa fedha ujao umakini utaongezeka kabla ya kutoa maamuzi
Mhe Renatus Mulunga, Mstahiki Meya wa Ilemela, amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa ushirikiano na muongozo wa kila siku ambayo imeifikisha Ilemela hapa ilipo huku akimuahidi kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa katika baraza.
Nikushukuru na kukuahidi ushirikiano wa kutosha na kutekeleza maelekezo yote uliyotupatia siku ya leo , kwani dhamira ni kuleta maendeleo kwa Manispaa ya ilemela, Mhe. Mulunga
Akiwasilisha Taarifa ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021 , Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Mhandisi Modest Apolinary, amesema kuwa pamoja na Halmashauri kupata hati safi kwa mwaka uliopita wa 2020/2021 Ilemela imeendelea kupata hati safi kwa kipindi cha miaka sita mfululizo ambapo hadi sasa hoja zilizobaki ni 11 tu.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.