Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, kupitia idara ya ardhi imetakiwa kuhakikisha inakamilisha majibu ya wananchi ambao wamesikilizwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza siku ya tarehe 17 oktoba 2023 akiwa katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Ilemela.
Maelekezo hayo yametolewa na Mhe. CPA Amos Makalla, mara baada ya kuhitimisha zoezi la kuwasikiliza wananchi waliofika kuwasilisha kero zao ambapo jumla ya wananchi 50 walisikilizwa
“Kila mwananchi aliyesikilizwa awe amejibiwa ndani ya siku 14, nataka kupima yale ambayo mkuu wa wilaya akiwaelekeza hamtekelezi, itakuwa jambo la ajabu sana iwapo malalamiko haya hayakufanyiwa kazi, niwaombe tekelezeni maelekezo haya yote tuliyoyatoa na majibu yapatikane ili tukija siku nyingine tuanze kusikiliza mambo mapya, nataka nikja Ilemela wananchi waseme yale uliyoagiza yamefanyiwa kazi”, alisistiza CPA Makalla.
Sambamba na maelekezo hayo amewataka watendaji wa idara ya ardhi kubadilika na kutoa huduma inayostahili kwa wananachi kwa kuwa lugha za kutoa huduma na matumaini kwa wananchi katika kutatua matatizo yao ya ardhi.
“Lugha za kuwahudumia wananchi ziwe lugha za staha na zenye matumaini sitaki kuja kusikia malalamiko ya namna mnavyowapokea wananchi wetu”,
Aidha amesema kuwa amebaini kuwa mambo yaliyochangia katika migogoro ya ardhi kwa kiasi kikubwa ni pamoja na upimaji shirikishi kwani inaonesha makampuni yanayopima hayana mawasiliano na ofisi, hayaratibiwi vizuri, lakini viongozi waliopo hawasimamii na kuwajibika ipasavyo katika suala hili la upimaji shirikishi.Hivyo ametoa maelekezo kwa Halmashauri kuhakikisha inalibeba jukumu hilo.
“Suala Kupima, Kupanga na Kumilikisha (KKK), ni jukumu la Halmashauri hivyo Ilemela hakikisheni mnajiridhisha na makampuni ya kupima , uwezo wake, mpango kazi wake,pamoja na kuhakiki kama michoro imezingatia maeneo ya huduma za jamii”, alihimiza CPA Makalla.
Aidha amewataka wataalam mhakiki madeni yote yanayohusiana na fidia za ardhi kwa watu waliotoa ardhi yao katika taasisi za serikali, wanaodai fidia katika mpango wa Kupima kupanga na kumilikisha (KKK) wanaodai fidia kupisha ujenzi au miundombinu yote yaainishwe yanayotokana na ardhi .
“Mstahiki Meya uwatake wataalam kuhakiki madeni yote ya ardhi kwani huwezi kutatua tatizo kama hujui ukubwa wa tatizo, ukishajua ukubwa wa tatizo utaweka mipango ya muda mfupi wa kati na mrefu katika kutatua matatizo” alisema CPA.Makalla
Nae mstahiki meya Mhe. Renatus Mulunga amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuendesha zoezi hilo la kusikiliza kero za wananchi huku akimuahidi ushirikiano sambamba na kutekeleza na kuyafanyia maelekezo kuyafanyia kazi ambapo amewataka watendaji kutimiza wajibu wao.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.