Tarehe 18 Septemba 2023, Mhe. CPA Amos Makalla , Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alizindua rasmi utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi (Ongea Live na Mkuu wa Mkoa) uzinduzi huo uliwajumuisha Wakuu wa Taasisi za Serikali pamoja na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakiwa na timu za menejimenti.
Akizindua utaratibu huo CPA Amos Makalla alisema kuwa utaratibu huo unaenda kuwapa wananchi nafasi bila mizengwe haki yao ya kusikilizwa kuanzia kwa mkuu wa mkoa hadi ngazi za chini kwa kutenga siku maalum ya kusikilizwa wananchi na kuwataka watendaji kujitahidi kero za wananchi zisifike mahakamani
Sambamaba na hayo amewataka watendaji wote kupitia uzinduzi huo kujifunza kuwa wananchi wana shida na ni muhimu kuimarisha usikilizaji wa kero katika Wilaya.
“Niwatake watendaji wa halmashauri zote leo iwe funzo, tubebe majukumu tuliyopewa na Mhe.Rais kila mkuu wa Idara ahakikishe anamsaidia mkurugenzi, kwa kushughulika na matatizo ya wananchi”. Alisema
Alihitimisha kwa kuwataka Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanaandaa utaratibu wa kusikiliza kero kata kwa kata, huku akihimiza kujielekeza kushughulika na matatizo hayo na kuyatolea maamuzi kwa masuala ya kiutawala na sio ambayo yapo mahakamani.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.