Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ndg. Ismail Ali Ussi ametoa rai kwa wafanyabishara wa soko la samaki la mwaloni Kirumba juu ya utunzwaji wa vifaa vya usafi ili viendelee kuweka mazingira ya Soko la Kimataifa la Samaki – Mwaloni lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela katika hali nzuri ya usafi.
Ametoa rai hiyo tarehe 26 /08/2025 wakati akikabidhi vifaa vya usafi, nakuzindua malori mawili na kijiko kimoja cha kubebea taka ikiwa ni miongoni mwa miradi iliyotembelewa na mbio za Mwenge wa Uhuru.
‘’Vifaa hivi tulivyokabidhi leo vitasaidia kuimarisha na kudumisha hali ya usafi katika soko hili, niwasisitize mvitunze ili usafi wa mazingira ya Soko uendelee kuimarika ” amesisitizaNdg. Ussi
Akisoma taarifa ya usafi na mpangilio wa soko kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Ndg. Johannes Buberwa amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana katika huduma ya usafi na udhibiti wa taka ngumu katika soko hilo ni pamoja na uhifadhi na utunzaji wamazingira kwa kudhibiti uzalishaji wa hewa inayotokana na taka zenye asili ya kibaiolojia, kudhibiti magonjwa ya mlipuko yanayotokana na taka na kuweka mazingira katika hali ya usafi wakati wote.
“Tunamshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuzingatia usafi wa mazingira katika masoko, barabara na mitaro ya maji katika Wilaya yetu” alimalizia Ndg. Buberwa
Vifaa vya usafi vilivyokabidhiwa pamoja na uzinduzi wa Malori 2 na Kijiko 1 cha kubebea taka vimegharimu shilingi 719.960 ambavyo vitasaidia kudumisha usafi katika soko hilo
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.