Prof.Tumaini Nagu ambae ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMIwa Ofisi ya Rais TAMISEMI amekagua vito vya kutolea huduma za afya vya Buzuruga na Buswelu samabamba na kupokea taarifa ya utendaji kazi wa idara ya Afya ndani ya manispaa ya Ilemela
Akikagua vituo hivyo siku ya tarehe 04 Julai 2025, Prof Nagu amewaelekeza watumishi wa kada ya afya kujitahidi kutoa huduma bora kwa ueledi na kuzingatia maadili ya taaluma yao na kuwataka kuangalia namna wanavyowasiliana kati yao lakini pia sana baina yao na wateja wanaowahudumia.
Aidha Prof Nagu amewapongeza watumishi wa idara ya afya kwa kazi kubwa wanayoendelea kufanya ya kuhudumia wananchi, na kusema kuwa serikali inatambua juhudi zao na jukumu hili kubwa la kuhudumia wananchi lakini ni dhahiri wanafanya kazi kubwa
Sambamba na hilo amempongeza mganga mfawidhi wa kituo cha buzuruga Dr. William Ntinginya kwa kuongeza mapato na kufanikiwa kuajiaro watumishi 20 kupitia mapato hayo ya kituo huku akimtaka mganga mkuu wa Mkoa kuhakikisha anafanya msawazo wa watumishi wa kada ya afya ili kuondoa changamoto ya upungufu wa watumishi na kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
"Tutaendelea kuhakikisha tunajenga miundombinu hapa katika kituo cha Buzuruga lakini pia kujenga vituo vya afya vya jirani ili kuwapunguzia idadi kubwa ya wagonjwa lakini pamoja na kuwaondolea wananchi adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya
Hali kadhalika Prof Nagu amewataka watumishi wa kada hiyo ya afya kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuendelea kutoa huduma bora na kuahidi kuzishughulikia changamoto walizoziainisha.
Akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi, Dr Maria Kapinga mganga mkuu wa manispaa ya Ilemela amezitaja changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikwamisha utendaji kazi wao kuwa ni pamoja na upungufu wa watumishi,nyumba za watumishi sambamba na baadhi ya vifaa tiba huku akimshukuru Naibu Katibu Mkuu huyo kwa kufika Ilemela.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.