Na Paschalia George, Afisa Habari Ilemela
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mhe. Nape Nnauye (Mb) amefungua mafunzo kwa njia ya mkutano wa video “video conference”yanayohusu mfumo wa utambuzi wa kaya na maeneo mbalimbali wa anwani za makazi na postikodi Tanzania.
Mafunzo haya yanafanyika kikanda ambapo mikoa mitatu kwa Tanzania baraTanga ,Mbeya na Ilemela –Mwanza ni wenyeji sambamba na Zanzibar kwa upande wa Tanzania visiwani.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Mhe. Nape amesema serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu inaendelea kutekeleza miradi ya kipaumbele ikiwemo mradi huu wa anwani za makazi.
“Nataka mradi wa anwani za makazi na postikodi ukaweke alama nchini kwa utekelezwaji wake wa viwango stahiki.Nitoe rai kwa yeyote mwenye mpango wa kukwamisha zoezi hili atupishe mapema atuache tutimize azma yetu njema kwa taifa letu” amesema Mhe.Nape.
Mhe.Nape ameongeza kuwa ni hitaji la serikali kuwa na mfumo huu ambao ni muhimu sana kwa jamii na serikali katika kupanga mipango ya kimaendeleo ya kiserikali sambamba na urahisi wa utoaji huduma mbalimbali za kijamii,kufungua masoko ya biashara za mtandaoni zenye tija na kama utatumika ipasavyo mfumo huo utaimarisha usalama na kuleta ajira zaidi kwa jamii yetu.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Elias Masala ambayo ndio wilaya wenyeji wa mafunzo haya kwa mkoa wa Mwanza amesema amepokea zoezi hilo kikamilifu na kuwahakikishia ulinzi na usalama wataalam wote wanaoshiriki zoezi katika kata zote 19 zinazounda manispaa ya Ilemela ambapo kata 4 kati ya hizo zitatumika kwa mafunzo ya vitendo kwa washiriki wote wa mafunzo haya kutoka mikoa 8 ya jirani.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.