Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe Angeline Mabula(MB) amesisitiza suala la uadilifu katika matumizi ya fedha za mkopo usiokuwa na riba uliotolewa na wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kupanga kupima na kumilikisha ardhi(KKK).
“Fedha hiyo mliyokopeshwa ikalenge katika lengo lililokusudiwa ili kuweza kuunga juhudi za Mhe. Rais za kufikia lengo lililokusudiwa ambalo ni kuondokana na changamoto na kero mbalimbali za ardhi ikiwa ni kumuwezesha mwananchi kumiliki ardhi kwani unapomuwezesha kumiliki kiwanja chake unampa fursa ya kupata mkopo katika benki, kuweka dhamana na uhakika na salama ya miliki yake”, alisema Mhe.Mabula
Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kikazi katika Manispaa ya Ilemela ambapo alipokea taarifa ya utekelezaji wa Idara ya ardhi pamoja na mawasilisho ya mpango kazi wa utekelezaji wa mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi huku akisisitiza kutokuwa na kisingizio chochote katika utekelezaji wa mradi huo.
Pamoja na hayo amesisitiza suala la ushirikishwaji ili kuweza kuwa na uelewa wa pamoja kwani utaenda kurahisisha zoezi zima katika utekelezaji wa mradi huu wa upimaji ardhi na kuongeza kuwa mafanikio ya mradi huu atapelekea wizara kuwatizama vizuri zaidi.
Aidha kuhusu suala la operesheni ya madeni ya ardhi amemtaka kamishna wa ardhi kuhakikisha kuwa anaratibu zoezi hilo kwa kushirikiana na halmashauri anazozisimamia na kuhakikisha kuwa kabla ya kuanza kudai madeni hayo matangazo yanatoka kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi.
Ndugu Elia Kamihanda ambae ni kamishna wa ardhi ameahidi kushirikiana na Manispaa ya Ilemela katika masuala ya ardhi hususan katika mradi huu kwa ajili ya kupanga, kupima na kumilikisha
Takriban kiasi cha Shilingi za kitanzania Bilioni 3.6 zimekopeshwa bila riba kwa Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu wa kupanga kupima na kumilikisha ardhi(KKK) uliotolewa na wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.