Katika kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “Ziro Malaria Inaanza na Mimi inaanza na wewe, Inaanza na sisi sote” Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 kupitia kiongozi wa mbio hizo Ndg. Ismail Ali Ussi umepongeza mchakato wa kutokomeza malaria katika Halmashauri ya manispaa ya Ilemela ikiwa ni pamoja wa uangamizaji wa mazalia ya mbu kwenye dimbwi lenye viluwiluwi wa mbu.
Akikagua mchakato huo siku ya Jumanne ya Tarehe 26.08.2025 Ndg. Ussi amesema kuwa amefurahishwa na jitihada za Wilaya pamoja na Halmashauri kwa ujumla kuona wanashirikiana kutokomeza malaria na kuhakikisha wananchi wanakuwa salama dhidi ya ugonjwa huo hatari.
Wilaya ya Ilemela imekuwa ikitoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Malaria na athari zake kwa jamii kupitia mabango na vipeperushi, vyombo vya habari na mikutano ya hadhara.
Kiwango cha maambukizi ya Malaria katika Wilaya ya Ilemela kimeendelea kupungua kutoka asilimia 5.4 mwaka 2023 hadi asilimia 2.5 mwaka 2024.
“ZIRO MALARIA INAANZA NA MIMI INAANZA NA WEWE, INAANZA NA SISI SOTE”
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.