Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2024 Ndugu Godfrey Eliakim Mnzava ametoa rai ya kufanyika kwa makongamano ya vijana kila robo ya mwaka wa fedha ili kutoa fursa ya kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu
Akizungumza wakati wa kufunga kongamano la vijana wa wilaya ya Ilemela lililofanyika katika viwanja vya TBA kata ya Kawekamo siku ya tarehe 13 oktoba 2024 kiongozi wa mbio hizo amesema kuwa ni maelekezo ya mbio za Mwenge 2024 kila wilaya kuhakikisha inafanya kongamano la vijana ili wapate fursa ya kuelezwa kwa kina mambo mbalimbali juu ya wapi tumetoka, wapi tupo na wapi tunaelekea ili kuwajengea uzalendo na kujua maslahi mapana ya taifa
'.. Natamani kuona makongamano ndani ya wilaya ya Ilemela Yana kuwa endelevu, Mara Kwa mara Vijana wakutane na waelezwe masuala mbali mbali na Kwa namna kongamano hili lilivyo sitalifunga badala yake nalihailisha ili tuendelee kuwa nayo mengine angalau yafike manne ..' Alisema
Aidha Ndugu Mzava ametamani kuona makongamano hayo ya vijana yanatumika kuwajengea uwezo vijana kutambua fursa za kiuchumi, kujitegemea na kuzitumia kujikwamua hao binafsi na taifa kwa ujumla
Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Ilemela ambae pia ni mratibu wa kongamano hilo Bi Amina Bululu amesema kuwa wilaya ya Ilemela ina fursa nyingi ikiwemo uwepo wa kuwa karibu na Ziwa Viktoria ambalo linaweza kutumika kujiinua kiuchumi kwa kufanya shughuli za uvuvi hivyo kuwataka Vijana kushirikiana na Serikali kuhakikisha fursa zote zinazopatikana zinatumika kikamilifu
Daktari wa afya ya akili kutoka hospitali ya rufaa ya Bugando Paul Ntemi akaongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wanapambana kuhakikisha Vijana wa taifa la Tanzania wanakuwa na afya ya akili iliyokuwa njema kwakuwa changamoto ya afya ya akili itachangia kulikosesha taifa Vijana wenye uwezo wa kuzalisha mali
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.