Mhe Renatus Mulunga ambae ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela amewataka wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu mbalimbali kuhakikisha kuwa wanavitunza vifaa walivyokabidhiwa kwani ni vya gharama kubwa.
Ameyasema hayo akiwa anakabidhi vifaa vilivyoletwa na OR-TAMISEMI kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum, na kusema kuwa umekuwa ni utaratibu wa serikali kutoa vifaa hivyo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
“Vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama kubwa hivyo niwaombe wazazi na walezi kuvitunza vizuri ili vidumu na vilete tija kwa wahusika”, Alisistiza.
Aliongeza kusema kuwa serikali inatambua uwepo wa watoto hawa, ikiwa ni pamoja na nguvu kazi yao katika kuleta maendeleo ndani ya jamii na kuwa serikali itaendelea kuwasaidia kadri baeti itakavyoruhusu.
Akwitelia Agustino, mzazi wa Philomena Haule (miaka 10) alisema kuwa mtoto wake ana ulemavu wa akili hivyo kiti hicho cha magurudumu (Wheel chair) itakuwa msaada sana katika kukaa pamoja na kusfiri mwendo mrefu zaidi hivyo ameishukuru serikali kwa kumpatia mtoto wake kiti hicho.
Nae mzazi wa mtoto Damian Domician mwenye umri wa miaka mitano ameishukuru serikali huku akiiomba kuendelea kuwafatailia mara kwa mara ili kuweza kujua mahitaji yao.
Akiwawakilisha wanafunzi wenzake, Isaya William (miaka 21) ambae ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wavulana Bwiru mwenye ulemavu wa miguu ameishukuru serikali kwa kumpatia magongo yatakayomrahisishia katika suala zima la masomo shuleni hapo.
Vifaa vilivyotolewa na OR-TAMISEMI vimejumuisha vifaa kwa ajili ya kundi la walemavu ambavyo ni vifaa vya kujifunzia na vifaa visaidizi kati ya vifaa hivyo ni kiti cha magurudumu (wheelchair), msgongo ys kutembelea, mafuta kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi pamoja na vifaa mbalimbali ikiwemo michezo ya watoto.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.