MRADI WA TAKA NI MALI WAZINDULIWA KATIKA MANISPAA YA ILEMELA
Mradi wa taka ni mali ulizinduliwa katika Manispaa ya Ilemela siku ya Jumamosi tarehe 28/10/2017 katika kata ya Kirumba.
Hafla ya uzinduzi wa mradi huo ilitanguliwa na zoezi la usafi katika kata hiyo Kirumba ikiwa ni utaratibu wa kila mwisho wa mwezi ambapo wadau mbalimbali wa mazingira pamoja na wananchi walishiriki zoezi zima la usafi.
Mradi wa taka ni mali, unafadhiliwa na kampuni ya Swiss contact ambapo lengo ikiwa ni kuhakikisha inasafisha mazingira na kutoa ajira kwa wananchi pamoja na kuwawezesha kwa kutoa elimu shirikishi juu ya utunzaji wa mazingira.
Vikundi mbalimbali vinavyojihusisha na utunzaji wa mazingira katika Manispaa ya Ilemela vilikabidhiwa vifaa vya usafi vilivyotolewa na kampuni hiyo ya Swiss Contact
Aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mhe Dr. Angeline Mabula (Mb) mbunge wa jimbo la Ilemela , amewataka wananchi wa Manispaa ya Ilemela kuona kuwa usafi ni sehemu ya maisha yao ya kila siku sambamba na kuagiza kuwachukulia hatua za kisheria wananchi wote wanaochafua mazingira .
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.