MRADI WA MAJI NYAMWILOLEWA KUNUFAISHA TAKRIBANI WANANCHI 12,056
Mradi huu wa usambazaji maji wa Nyamwilolelwa unatarajia kunufaisha zaidi ya wananchi 12,056 kutoka mitaa ya Shibula, Kihiri, Nyamwilolelwa, Semba A, Semba B, Muhonze A na Muhonze B.
Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela, Ndugu John Wanga amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo 30.01.2018 na mpaka sasa zaidi ya asilimia 70 ya utekelezwaji wake umekamilika.
Aidha amewaomba wananchi wanufaika wa mradi huo na viongozi wa maeneo husika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji kwa kuutunza mradi huo na kutoa ushirikiano ili uweze kukamilika kwa wakati.
Huku akiwahakikishia wananchi wake kuwa manispaa yake itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji na huduma nyingine za kijamii ili kuhakikisha inatatua changamoto na kero zinazowakabili wananchi waManispaa ya Ilemela.
Mkandarasi Edge Point Co. Ltd anayehusika na usambazaji wa mabomba ya usambazaji maji wa mradi huo anaendelea na kazi hiyo. Ambapo mkandarasi Ms Jassie & Company alihusika na ujenzi wa matanki ya maji yenye lita za ujazo 225,000.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.