Kukamilika kwa ujenzi wa kisima cha maji safi katika stendi ya mabasi ya Nyamhongolo kilichogharimu shilingi Mil. 26.85 fedha za mapato ya ndani ya manispaa ya Ilemela kinatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya wakazi 3160 wa maeneo hayo na jirani.
Kisima hiki ambacho lengo lake ni kupunguza ukosefu wa maji na kuwezesha upatikanaji wa maji ya uhakika katika kituo hicho pamoja na maeneo jirani kama vile Hosteli na Zahanati ya Nyamhongolo kilizinduliwa rasmi na Mwenge wa Uhuru 2025
Akizindua mradi huo tarehe 26.08.2025, kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka Ndg. Ismail Ali Ussi alimpongeza mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Bi Ummy Wayayu kwa kubuni mradi huu wa kisima cha maji safi na salama katika stendi hii ya mabasi Nyamhongolo kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji katika eneo hilo.
Aidha Ndg Ussi amewataka watumiaji wa kisima hicho kutunza miundombinu iliyowekwa ili iweze kudumu na kuwa msaada kwa jamii ya sasa na vizazi vijavyo.
Kisima hiki chenye uwezo kuzalisha lita 8000 kwa siku ambapo mahitaji ni lita 3600 hivyo kuwa na ziada ya lita 4400 kinaenda kunawahakikishia wakazi wa maeneo hayo upatikanaji wa maji ya uhakika na kupunguza gharama za ulipiaji wa maji katika Kituo cha Mabasi na Maegesho ya Malori na zahanati ya Nyamhongolo sambamba na utunzaji mzuri wa mazingira kwa sababu ya uwepo wa maji ya uhakika.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.