Viongozi wa Mtandao wa kitaifa wa wanawake wanaoishi na VVU nchini Tanzania wenye usajili wa Namba 00NGO/R/3522 wakiongozwa na Bi Veronica Lymo ambae ni Mkurugenzi wamefika ofisni kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela na kuutambulisha na kuzindua mradi wa COMPASS AFRICA
Ambapo zoezi la uzinduzi wa mradi huo limetekelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bi Neema Semwaiko.
Bi Neema amewataka washiriki ambao ni wasimamizi wa vituo vya kutolea huduma za afya na jamii kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa mtandao huo ili kufanikisha lengo lililokusudiwa ambalo ni kupunguza maambukizi ya VVU kwa watoto wachanga.
Mradi huu utajikita utafiti ili kupunguza maambukizi ya VVU kwa watoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi 14, mama wajawazito na wale wanaonyonyesha, wamama wanaoishi na VVU wa Ilemela,alisema Bi Veronica Lymo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.