Ujenzi wa mradi wa BITEC (Bwiru Information Techology Education Centre), ni mradi uliotekelezwa na mfadhili SOGEA SATOM (Issa) ambapo amejenga jengo la TEHAMA ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu ya ufundishaji wa elimu ya Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA kama kompyuta mpakato (laptop) 35, zenye thamani ya sh. Milioni 24, pamoja na samani za meza ukiwa umegharimu fedha za kitanzania shilingi Milioni 102.59
Takriban wanafunzi zaidi ya 3000 wa shule mbili za msingi za Mnarani na Bwiru, shule mbili za sekondari za kata za Kitangiri na Mnarani sambamba na shule mbili kongwe za sekondari za kulala za Bwiru wavulana na wasichana katika kata ya Pasiansi.
Manufaa yatakayopatikana kupitia mradi huu ni pamoja na kurahisisha matumizi ya mifumo mbalimbali ya utendaji kazi kama vile FFARS, PEPMIS, PREM, BEMIS, NEST ambayo inahitaji kuwa na mtandao wa internet
Aidha kufuatia kuanzishwa kwa tahasusi mpya ya PMCS (Physics, Mathematics Na Computer Science) katika shule za Bwiru wavulana na wasichana wanafunzi hao watatumia kituo hicho kwa ajili ya mafumzo
Mradi huu umezinduliwa rasmi na Katibu Tawala wa Wilaya yaa Ilemela Bi Mariam Msengi ambapo amewashukuru wafadhili wa mradi kwani kupitia mradi huu wanafunzi wanaenda kuongeza uelewa wa TEHAMA ukizingatia hizi ni zama za kidigiti
Bi Mariam Msengi amewataka walimu wakuu na wakuu wa shule zote zitakazonufaika na mradi huo kuhakikisha wanaitunza na kuilinda miundombinu hiyo ili itumike na vizazi vinavyokuja.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.