Watumishi wa kituo cha afya Buzuruga wamepewa motisha ya kiasi cha shilingi laki tano kama ishara ya kutambua, kuthamini na kupongeza kazi nzuri wanazozifanya katika kuwahudumia wananchi .
Akizungumza katika kikao chake na watumishi wote wa idara ya afya manispaa ya Ilemela katika kituo cha afya Buzuruga mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Bi. Ummy Mohamed Wayayu amewapongeza watumishi wa kituo hicho pamoja na kuwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii bila kujali maslahi binafsi kwa kuwa kazi wanayoifanya ni ya wito wa ki Mungu .
"... Inawezekana mkafanya kazi wengi alafu akatambulika mmoja wenu, Hiyo isiwavunje moyo sifa ya taasisi huwa ni ya wote, mie kama mkurugenzi wenu nitawapa laki tano tufanye kazi raha ya kufanya kazi kwa bidii siku zote huwa inalipa..." alisema
Aidha Bi.Wayayu ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zote zilizowasilishwa na wataalam wa kituo hicho cha afya ikiwemo upungufu wa afisa tehama wa kituo na afisa ugavi ili kuongeza ufanisi wa kazi katika kituo hicho .
Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya ya Ilemela Daktari Maria Kapinga mbali na kumshukuru mkurugenzi huyo kwa namna anavyounga mkono juhudi za watumishi wa idara ya afya amewataka watumishi wachache wa kituo hicho wanaolalamikiwa na baadhi ya wananchi kuongeza juhudi na uzalendo katika kazi ili kuendelea kukipatia sifa kituo hicho pamoja na kuondoa malalamiko kwa wananchi .
Suleiman Baruani ni muhasibu wa kituo hicho ambapo ameomba kujengewa uwezo juu ya mifumo mipya ya fedha na ugavi ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi wakati mganga mfawidhi wa kituo hicho Dkt. Ndinginya akiomba kuongezwa kwa majengo ili watumishi waweze kuenea katika vyumba vya kutolea huduma .
Akimkaribisha mkurugenzi, Afisa utumishi Mkuu wa manispaa ya Ilemela Ndugu Egidy Teulas amewapongeza watumishi wa kituo hicho huku akiwaasa kuzingatia taratibu, sheria na kanuni za utumishi wa umma katika uwajibikaji wao .
Mkurugenzi Ummy alitumia nafasi hiyo pia kutembelea mazingira ya kituo hicho pamoja na kukagua utoaji wa huduma kwa wananchi huku akiahidi kuendelea kufanya hivyo katika vituo vyengine vya kutolea huduma za afya .
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.