Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Bi.Ummy Wayayu amewataka maafisa maendeleo jamii kuhakikisha wanawajibika katika maeneo yao ya kazi kwa kutoa elimu mbalimbali na kuhamasisha jamii ya Ilemela kushiriki katika masuala mbalimbali.
Ameyasema hayo tarehe 27 Februari 2025, wakati akikabidhi spika kwa maafisa maendeleo ya jamii wa kata zote 19 ikiwa nii utekelezaji wa waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Mohamed Mchengerwa alilolitoa mwaka 2024 la kuhakikisha kuwa wakurugenzi wa halmashauri wanawanunulia maafisa wa maendeleo ya jamii wa kata spika hizo ili kurahisisha kazi yao ya uraghibishi.
"..Tuwe msaada kwa watu wetu, mwananchi akihitaji kusaidiwa kufahamu kitu asaidiwe wala msiombe chochote kutoka kwake.." Amesema Mkurugenzi Ummy
Sambamba na hilo amewataka maafisa maendeleo ya jamii kufuatilia kwa karibu masuala ya marejesho ya mikopo ya 10% inayotolewa na Halmashauri ili kufanya zoezi la ukopeshaji kuwa endelevu.
Ndugu Majura Mgeta ambae ni afisa maendeleo ya jamii kutoka kata ya Sangabuye, kwa niaba ya maafisa wote amemshukuru mkurugenzi kwa kukutana nao na kumuahidi kutekeleza maelekezo aliyotoa huku akiwasilisha ombi la kupatiwa usafiri hususan kwa waliopo kata za mbali
Nae Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii Ndugu Mohammed Atiki amehitimisha kwa kumhakikishia mkurugenzi kuyasimamia maelekezo aliyoyatoa na kuwataka maafisa maendeleo ya jamii kuvitumia vitendea kazi hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.