Mkurugenzi Ummy Wayayu amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa hatua mbalimbali za miradi ilipofikia.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi akiambatana na wakuu wa idarabza halmashauri, alikagua miradi 12 ya sekta ya afya na elimu yenye thamani ya takriban shilingi milioni 941 fedha kutoka serikali kuu na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi Ummy alitoa maelekezo kwa wasimamizi wa miradi kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati sambamba na kuhakikisha kuwa fedha walizopatiwa zinakamilisha ujenzi kwani hakuna nyongeza ya fedha itakayotolewa.
Amehitimisha kwa kuwataka wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha wanatunza vizuri nyaraka mbalimbali za ujenzi na kuhimiza kila mmoja kusimama katika nafasi yake wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.