• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Maadili ya Msingi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utumishi na Utawala
        • Mipango na ufuatiliaji
        • Kilimo, Ufugaji na Uvuvi
        • Maendeleo ya Jamii
        • Elimu Sekondari
        • Elimu ya Awali na Msingi
        • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
        • Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Miundombinu na Uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Vitengo
        • Mazingira na Usafishaji
        • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
        • Michezo, Utamaduni na Sanaa
        • Fedha na Uhasibu
        • Sheria
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Manunuzi
        • TEHAMA na Takwimu
        • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MKURUGENZI ILEMELA ATOA WITO, "TUKATENDE HAKI KWA WANANCHI WETU"

Posted on: December 2nd, 2022

Wito umetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Mhandisi Modest Apolinary kwa wajumbe wa mabaraza ya usuluhishi ya kata kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi ili kuweza kupunguza malalamiko yanayotoka kwa wananchi.


Mhandisi Modest ametoa wito huo wakati wa zoezi la kuwaapisha na kutoa mafunzo kwa wajumbe hao wa mabaraza ya usuluhishi ya kata

“Niwaombe mkatende haki, msiende kutumia fedha za wale wenye nazo kuchukua ardhi ya wale wasio na fedha ili wote kwa pamoja tupunguze malalamikio ya wananchi,nyie mnajua haki kwasababu ni wenyeji wa maeneo hayo mnajua historia ya maeneo yenu mnajua mwenye haki ni nani kwanini mwenye haki ananyimwa haki anapewa asie na haki”, Amesisitiza Mkurugenzi.


Pamoja na wito huo, Mhandisi Modest ameweka bayana kuwa iwapo itabainika kuwa iwapo miongoni mwa mabaraza haya itabainika hayatendi haki na kujiridhisha basi hatosita kuyavunja na kutafuta viongozi wengine wataoendana na taratibu huku akitoa mfano kwa baraza la kata la Kirumba ambalo lilivunjwa baada ya kubainika kwa vitendo vya rushwa.


Aidha amewataka wajumbe hao kuanza kazi mara moja baada ya kuapishwa kwani wananchi wanasubiria kusuluhishwa migogoro yao. Sambamba na hilo amesemea kuwa Ilemela zipo changamoto kubwa za migogoro ya ardhi ambayo iko kwao hivyo angependa kuona  wananchi wanapokuja kulalamika kwake wanakuja na maoni ya mabaraza ja,mbo ambao pia litamsaidia Mwenyekiti wa baraza la ardhi la wilaya kutoa hukumu iliyo sahihi.

Wakili Patrick Muhere ambae ni Mwanasheria wa Manispaa, kabla ya kuwaapisha wajumbe hao  amewaelekeza kuwa kazi yao  kubwa ni kusuluhisha na sio kutoa maamuzi na kufafanua zaidi kuwa mabaraza kazi yake ni kusikiliza malalamiko ya wadaawa (ambao ni mlalamikaji na mlalamikiwa) wanasemaje, na kusisitiza kuwa hawaendi  kufanya maamuzi  kwani kwa kufanya hivyo watawaingiza kwenye gharama kwani wakikata rufaa kwa Mwenyekiti hukumu itafutwa na ataangalia kama hatua zilifuatwa

“Kazi yenu kubwa ni kusuluhisha na sio kutoa maamuzi, baraza kazi yake ni kusikiliza malalamiko ya wadaawa ambao ni mlalamikaji na mlalamikiwa wanasemaje hivyo hatufanyi kwa utashi bali tunafanya kwa mujibu wa sheria”, amefafanua wakili Muhere


Ndugu Mayeye Magambo Mwenyekiti wa baraza la ardhi la nyumba mkoa wa Mwanza ametoa angalizo kwa wajumbe hao kuwa sheria ya mabaraza ya kata imetoa siku 30 kuwa wamefanya  usuluhishi na iwapo pande mbili zitakuwa hazijaridhika hawatatakiwa kukata rufaa bali wapewe hati ya kukosa usuluhishi na wafike baraza la wilaya ambapo watawasikilizwa kwa kuita mashahaidi baada ya kufungua maombi.

Ndugu Mayeye amewahimiza kuwa kazi yao ni kusikiliza pande zote mbili kwa kutumia busara na hekima na wahakikishe wanatumia vipawa walivyojaaliwa na Mwenyezi Mungu katika kuwapatanisha watu wenye migogoro na kumaliza migogoro kwa amani na upendo ili amani iendelee kudumu katika kata na watu waendelee kuishi bila migogoro.


Asia Mkandala na ndugu Mchunguzi ni wajumbe kutoka mabaraza ya kata za Nyamanoro na Pasiansi wao wameshukuru kwa kuapishwa kwao na kupewa mafunzo mafupi na kuahidi kuwa watatenda kazi kutokana na miongozo bila kukiuka maelekezo waliyopatiwa kwa kushirikiana na wajumbe wenzao kutekeleza majukumu yao ya usuluhishi kwa kutenda haki bila ya upendeleo wowote na bila kuvuka mipaka ya miongozo kwa hekima na busara huku wakiishukuru serikali kwa kuwapunguzia majukumu ya mabaraza.


Wajumbe 141 wa mabaraza ya usuluhishi ya kata wameapishwa ambapo jukumu kubwa la mabaraza haya ni kusuluhisha migogoro ndani ya kata zao inayohusiana na ardhi, ndoa na kushughulikia makossa ya jinai yatokanayo na ukiukwaji wa sheria ndogo za Halmashauri.




Announcements

  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2022 SHULE ZA SERIKALI NA BINAFSI MANISPAA YA ILEMELA January 29, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAPOKEZI YA FEDHA September 30, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KATIKA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA JULAI-SEPTEMBA 2022 October 11, 2022
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2022 December 01, 2022
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • DC MASALA AAGIZA UFUATILIAJI KWA WANAFUNZI AMBAO HAWAJARIPOTI

    February 06, 2023
  • ILEMELA YAKIDHI VIGEZO VYA KUTEKELEZA MIRADI MINNE

    January 19, 2023
  • ELIMU YA MATUMIZI BORA YA FEDHA YATOLEWA KWA WANUFAIKA WA MKOPO WA ASILIMIA 10

    January 18, 2023
  • DC ILEMELA APIGA MARUFUKU MICHANGO KIDATO CHA KWANZA

    January 17, 2023
  • Tazama zaidi

Video

SHULE YA SEKONDARI BUZURUGA ILIYOJENGWA KWA FEDHA ZA SEQUIP
More Videos

Quick Links

  • Kuhakiki Taarifa za Mpiga Kura
  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip
  • Maombi ya leseni ya biashara

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.